Zaidi ya wakazi elfu sita wa wilaya mpya ya Malinyi mkoani Morogoro wanakosa huduma muhimu za kijamii ikiwemo elimu, afya na mahitaji mengine ya kawaida ikiwemo vyakula na bidhaa, baada ya kukatika kwa mawasiliano ya barabara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na ujenzi uliosimama wa makalavati katika maeneo mbalimbali.
ITV imetembelea maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo na kushuhudia hali hiyo, ikiwemo katika eneo la Butu kijiji cha Tanga, ambapo mawasiliano ya upande mmoja wa kwenda vijiji vilivyopo tarafa ya Ngoheranga yamekatika baada ya mkandarasi aliyekuwa akijenga kipande cha barabara ya Lupiro-Malinyi hadi Kilosa kwa mpepo inayosimamiwa na Tanroads kuitelekeza barabara hiyo kutokana na mvua, hali iliyosababisha maji kuzingira eneo hilo na wakazi kushindwa kuvuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine, isipokuwa kwa kutumia matrekta au pikipiki ambazo pia hupita kwa tabu eneo hilo, huku wajawazito,wagonjwa na wafanyabiashara wakiathiriwa zaidi na hali hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi Said Msomoka na mbunge wa jimbo la Malinyi Dk Haji Mponda pamoja na kukiri changamoto iliyopo ya barabara katika maeneo mengi ya wilaya hiyo, sambambà na mazao kuathiriwa na maji kutokana na kufurika kwa mto Furua unaohitaji kujengewa tuta, wamesema suluhsho la kudumu la changamoto hizo ni kuanzishwa kwa mkoa mpya utakaozijumuisha wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero, pamoja na ulipaji haraka wakandarasi na malipo, masharti na vigezo vya tenda kuzingatia hali halisi ya maeneo badala ya unafuu wa gharama unaofanya wakandarasi wasio na uwezo kukubali tenda na kushindwa kuzimudu.
Mkuu wa wilaya ya Ulanga anayesimamia pia wilaya mpya ya Malinyi Christina Mndeme amekiri serikali kutambua tatizo hilo na tayari wakandarasi wamerudi katika baadhi ya maeneo kuendelea na kazi hivyo kuwasihi wananchi kuwa na subira kwa kipindi hiki.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment