Wafanyabiashara wanne wa Tanzania wameuwa kwa kupigwa risasi kisha kuchomwa kwa vitu vyenye ncha kali nchini Msumbiji baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe alisema tukio hilo lilitokea usiku wa Jumatatu iliyopita katika machimbo ya dhahabu, Kijiji cha Mtoro Mtupweshi Kamprigando.
Aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Salum Mfanga (44) Mkazi wa Temeke, Dar es Salaam, Yusuph Twalibu (34) na Mariam Ramadhani (30) wakazi wa Tanga na Hamisi Mkapira (40) wa Morogoro.
Kamanda huyo alisema kifo cha Mariam ambaye alifanikiwa kujiokoa, kilisababishwa na kukosa huduma ya haraka baada ya kuvunjika mguu.
Kamanda huyo alisema wafanyabiashara hao walivamiwa na majambazi waliokuwa na risasi pamoja na mapanga katika vibanda vya kubadilishia fedha nchini humo. “Miili ya wafanyabiashara hao ililetwa na ndugu zao ambao wanaishi Msumbiji,” alisema.
Wakizungumzia tukio hilo, Said Mfanga na Dotto Ramadhani ambao ni ndugu wa marehemu hao walisema baada ya kuwaua, majambazi hao waliwapora fedha pamoja na mabegi yao.
MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment