Featured
Loading...

Diwani wa Kimwani Kagera auwawa kinyama kwa kushambuliwa na kundi la watu wenye silaha za jadi.

Diwani wa kata ya Kimwani Bw. Silvesta Mringa mkazi wa kijiji cha Kaguramo wilaya ya Muleba mkoani Kagera ameuwawa kinyama kwa kushambuliwa na kundi la wahalifu wenye silaha za jadi ambao wamekamatwa mda mchache baada ya tukio na kukutwa wakiwa na kitita cha fedha hali iliyosababisha wananchi kuvamia kijiji cha Kiziramyaga daraja nane wanapoishi watuhumiwa wa mauaji hayo na kuteketeza kwa moto nyumba nane, mashine mbili za kusaga nafaka, mashamba kuhalibiwa kinyume cha sheria za nchi.
Tukio hilo limetokea katika vijiji viwili kata ya Kimwani ambapo mauaji yametokea nyumbani kwa marehemu kijiji cha Kaguramo na uhalibifu wa mali za watuhumiwa wa mauaji zimehalibiwa katika kijiji cha Kiziramyanga eneo la daraja nane ambapo inadaiwa kuwa usiku wa majira ya saa mbili Bw. Slvest ambaye kwa sasa ni marehemu akiwa anaangalia taarifa ya habari kwenye runinga watu wasiojulikana walipisha hodi nyumbani kwake na alipofungua mlango walimvamia na kumshambulia ambapo alifariki dunia baada ya kufikishwa hospitali ya Kagondo kama wanavyobainisha ndugu na mkewe.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji Busindi Bw. Mustafa  Samson ameelezea jinsi wananchi walivyomkamata mhalifu wa mauaji ya kinyama aliyelipwa ujira wa shilingi 1,500,000 huku afisa mtendaji wa kata ya Kimwani Bw. Martine Tibaigana akibainisha uhalibifu wa mali za watuhumiwa wa mauaji hayo.
 
Kufuatia hali hiyo serikali ya wilaya ya Muleba ikalazimika kufika eneo la tukio ambapo kamati ya ulinzi na usalama ikajionea hali halisi ya uhalibifu wa mali za watu ambapo katibu tawala akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo amewaasa wananchi kuacha tabia ya kuchukua sheria mikononi huku kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw.Agastine Oromi akizungumza na ITV kwa njia ya simu amesema watu watatu wamekamatwa huku wengine wanne wakitafutwa kutokana na tukio hilo. 

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top