Featured
Loading...

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Akutana Na Mabalozi Wa Qatar Na Kuwait Leo

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi wawili kutoka nchi za Qatar na Kuwait. 

Akizungumza kwa nyakati tofauti na mabalozi hao leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu amewashukuru mabalozi hao kwa pongeza walizokuja kumpatia, pamoja na namna ambavyo nchi zao zimekua zikisaidia Tanzania, ambapo ameahidi  kuendeleza ushirikiano mzuri  baina ya Tanzania na nchi zao.

Kwa upande wake, Balozi wa Qatar, Abdallah Jassim al Maadad amesema  Serikali yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo yote ambayo Qatar imepiga hatua kubwa na inaweza kutoa msaada kwa Tanzania.

Amesema Quwait iko tayari kuwekeza nchini katika sekta ya  kilimo, kwa vile ardhi ya Tanzania ni yenye rutuba na inafaa kwa shughuli za kilimo. Aidha, ametaja sekta nyingine  ambazo wangependa kuwekeza ni  pamoja na sekta ya uvuvi na viwanda.

Naye, Balozi wa Kuwait, Jasem Al Najem ambaye amekuja kujitambulisha kwa Waziri Mkuu, amesema nchi yake kupitia ‘Kuwait fund’ iko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Balozi  Najem, pia ameshauri vituo vya uwekezaji vya Tanzania na Kuwait kufanya kazi kwa ushirikiano zaidi ili kurahisisha utekelezaji wa miradi mbalimbali.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top