Featured
Loading...

Taarifa kwa wote watakaokaidi kupisha gari la zima moto

Image result for naibu waziri charles kitwanga
Taarifa kwa wote watakaokaidi kupisha gari la zima moto
Katika kuhakikisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linafanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika kupambana na majanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ameliagiza jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakayekaidi kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji pindi linapokuwa linawahi eneo la tukio ili kuweza kuzima moto na kuokoa maisha ya watu pamoja na mali zao.
Waziri Kitwanga ametoa agizo hilo alipokuwa anamaliza ziara yake katika Makao Makuu ya Jeshi hilo Kanda ya Ilala, Dar es Salaam mara baada ya Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kamisha Jenerali, Pius Nyambacha kubainisha kuwa mojawapo ya changamoto zinazolikumba jeshi hilo ni ukaidi wa baadhi ya wananchi kutotaka kupisha gari la Zimamoto pindi linapokuwa katika harakati za kuwahi eneo la tukio.
“Hivi hamjui hata msafara wa Rais unalazimika kupisha gari la Zimamoto au wagonjwa? Iweje leo wananchi wasipishe magari hayo? Simamieni sheria hii” Alisisitiza Mhe. Waziri.
Aidha Mhe. Waziri aliahidi kushughulikia changamoto zote zinazolikabili Jeshi hilo changamoto hizo ni ukosefu wa vifaa, ufinyu wa bajeti pamoja na idadi ndogo ya Askari.

MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.

ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top