Madereva wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam wamesema watagoma kuendesha magari hayo kufuatia uongozi wa mabasi hayo kuwapa mkataba wa kazi usiokidhi mahitaji.
Baadhi ya mahitaji hayo ni mshahara mdogo wa shilingi laki 4 kwa mwezi tofauti na makubaliano ya awali ya shilingi laki 8.
Wakiongea na Kurasa leo madereva hao wamesema pia wameshangazwa na kitendo cha uongozi wa mabasi hayo kuwapa mkataba wa kazi bila ya kuwapatia nakala yake jambo ambalo wamesema ni kinyume cha taratibu za ajira.
Madereva hao ambao leo walikusanyika katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo haraka kilichopo eneo la Kamata wamesema tayari walishatangaziwa malipo halisi kuwa ni shilingi laki 8 hivyo kitendo cha kusainishwa mkataba wa malipo ya shilingi laki 4 hawakubaliani nacho
MAAJABU YA MTANDAONI BOFYA HAPO CHINI HUTAAMINI MACHO YAKO.
ABOUT PRINCE BEWISA: PRINCE BEWISA BLOG is an independent organization which belongs to Bewisa Multimedia and Communication (BMC Media). Prince Bewisa was officially established on September 25, 2013 for the purpose of publishing Social contents that benefits to every visitor and community in general. It’s social blog for News, Entertainments, Education, Sports, Articles, and Business.
Post a Comment