Featured
Loading...

Mugabe: 'Mtakiona' Trump

Image result for Robert MugabeRais wa Zimbabwe Robert Mugabe amewaambia maseneta wa Marekani waliozuru taifa hilo kwamba watajutia kutofanya urafiki naye iwapo Donald Trump atachaguliwa kuwa rais katika uchaguzi wa mwezi Novemba.
Maseneta hao Chris Coons na Adam Schiff waliambia gazeti la Politico nchini Marekani kwamba walikuwa katika taifa hilo kuzungumzia kuhusu usafirishaji wa wanyama mwitu na kwamba waliomba kukutana na rais huyo na wakashangaa kwamba alikubali kuonana nao.
Maseneta hao wamesema kuwa Mugabe aliwataka kuelezea kwa nini Marekani inaliwekea vikwazo taifa hilo ambapo walitoa sababu kadhaa.
Ni wakati huo ambapo bwana Mugabe aliwaambia: ''Wakati Trump atakapokuwa rais mutatamani mungefanya urafiki nami''.

Programu Ya Kampeni Za Hillary Clinton Yadukuliwa

Image result for Hillary ClintonMaafisa wa upelelezi nchini Marekani wamesema kuwa programu ya komputa inayotumiwa na jopo linalosimamia kampeni ya Bi Hillary Clinton imedukuliwa.
Mameneja wanaosimamia kampeni ya Bi Clinton walisema kuwa wadukuzi hao wameingilia mawasiliano katika kompyuta hiyo.
Awali kamati ya jopo hilo inayosimamia ukusanyaji pesa za kampeni ilisema kuwa mawasiliano yake yalikuwa yamedukuliwa.
Vyombo vya habari Marekani vinasema kuwa udukuzi huo huenda unahusika na shughuli za upelelezi za Urusi.Image result for Hillary Clinton
Shirika la upelelezi la Marekani la FBI nalo linasema kuwa linaendelea na uchunguzi kuona iwapo makundi mengi zaidi yanaendesha udukuzi huo dhidi ya kompyuta za chama cha Democratic.
Juma lililopita mtandao wa kufichua habari za siri wa Wikileaks, unaodhaniwa kuwa na uhusiano mkubwa na Urusi ulifichua barua pepe nyingi kuhusiana na chama cha Democratic.

Malik Nduguye Obama kumpigia kura Donald Trump

Image result for Bw Malik amesema angependa sana kukutana na Bw Trump                    Malik Obama alikutana na Obama mara ya kwanza 1985.
Nduguye wa kambo wa Rais wa Marekani Barack Obama, Malik, ametangaza kwamba atampigia kura mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump.
Malik ameamua kutounga mkono chama cha Democratic chake Rais Obama ambacho mgombea wake ni Hillary Clinton.
Amesema anampenda sana Bw Trump kutokana na “uwazi wake” na kuongeza kwamba amesikitishwa sana na uongozi wa Rais Obama.
Ameambia BBC kwamba anaamini BwTrump, ni mtu mwenye huruma, mkweli na mwenye ushawishi.
"Akizungumza kwenye runinga anaonekana mtu anasemaye ukweli, kuhusiana na dunia kwamba imeharibika na hakuna usalama,” amesema Bw Malik.
Malik, 58, kwa muda mrefu alikuwa mfuasi wa chama cha Democratic lakini anasema utawala wa nduguye umemfanya kubadilika na kuanza kuunga mkono Bw Trump.
Akizungumza awali na gazeti la New York Post la Marekani, Malik alisema jambo lililomtamausha zaidi ni hatua ya mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani FBI James Comey kupendekeza Bi Clinton asishtakiwe kutokana na hatua yake ya kutumia sava ya kibinafsi ya barua pepe akiwa waziri wa mambo ya nje.
Hajafurahia pia kwamba Bi Clinton na Rais Obama waliongoza vita vilivyopelekea kuuawa kwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi ambaye anasema ni mmoja wa marafiki zake wakuu.
Pia, hafurahishwi na hatua ya chama cha Democratic cha Marekani kuunga mkono ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
“Nampenda Donald Trump kwa sababu anazungumza kutoka moyoni. Ningependa kukutana naye,” anasema.
Baba yao Barack Obama Sr., aliondoka Kenya mwaka 1959 Malik alipokuwa na umri wa mwaka mmoja na akajiunga na chuo kikuu cha Hawaii, ambapo alikutana nan a baadaye akamuoa mamake Rais Obama, Stanley Ann Dunham.
Image copyrightAP

Wawili hao hata hivyo wamekuwa wakigombana. Malik amekuwa akimshutumu nduguye akisema hajakuwa akimsaidia.
Malik aliwania ugavana Siaya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 lakini akashindwa.
Amesema amejiandikisha kama mpira kura katika jimbo la Maryland na anapanga kupiga kura mwezi Novemba.
Bw Malik amesema hakuna uhasama mkubwa kati yake na Rais Obama lakini hamuamini sana. Amesema wakati Rais Obama alipokuwa akiomba kura alizungumza sana zake Kenya lakini alipoingia uongozini hajakuwa akiwasiliana nao sana.

Programu Za Vyuo Vikuu Ambazo Hazijasajiliwa Na TCU Na NACTE Kufutwa

Image result of Bi.  Maimuna PostmanKatibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Bi. Maimuna Tarishi ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)   kufuta programu zinazotolewa na vyuo vikuu hapa nchini ambazo hazijafanyiwa tathmini wala kusajiliwa.

Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo leo alipokuwa akifunga maonyesho ya kumi na moja ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Julai 20 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

“Wakati mwingine najiuliza inakuwaje chuo kinafundisha programu ambayo haijatathminiwa wala kusajiliwa na TCU au NACTE, ni lazima tuwe makini kwani tunahitaji elimu bora katika vyuo vyote nchini bila kuangalia kama ni cha Serikali au ni Binafsi,” alifafanua Bi. Tarishi.

Aliendelea kwa kusema kuwa, TCU na NACTE wanajukumu ya kuzifuta programu hizo na kuanzisha programu zenye uhitaji mkubwa kama vile shahada ya mafuta na gesi, Kompyuta na Ualimu wa Sayansi ambapo wataalamu katika maeneo hayo wamekuwa wakihitajika zaidi katika kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya Tano inajikita zaidi katika uanzishwaji wa viwanda.

Aidha Bi. Tarishi amewataka TCU na NACTE kudahili wanafunzi wenye vigezo vinavyohitajika na kusisitiza kuwa ni bora kuwa na wanafunzi wachache katika vyuo vikuu kuliko kuwa na wanafunzi wengi ambao hawana sifa.

Wakati huo huo Mkuu wa Kitivo cha Biashara Chuo Kikuu cha Zanzibar Salehe Mwinyi amesema kuwa wanafunzi wengi wamejitokeza kutembelea banda la Chuo hicho kutaka kujua pogramu zinazotolewa na wengi wao wameonyesha nia ya kujiunga katika Chuo hiko.

Vile vile Mwinyi amesema kuwa mwaka huu idadi ya wanafunzi waliotembelea maonyesho hayo ni wengi zaidi kutokana na eneo lililochaguliwa kufikika kwa urahisi kutoka pande zote za jiji la Dar es Salaam ukilinganisha na mwaka jana ambapo yalifanyika viwanja vya Saba Saba na kutembelewa na idadi ndogo ya wanafunzi na wazazi.

Kwa upande wake, Fadia Suleiman mwanafunzi anayetegemea kujiunga na Chuo Kikuu mwaka huu, amesema kuwa maonyesho hayo yamemsaidia kwa kiasi kikubwa kujua ni programu gani asome kutokana na ufaulu wake wa kidato sita.

Maonyesho ya  Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ambayo huandaliwa na TCU hufanyika kila mwaka yakitoa fursa kwa Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi kutoa elimu kwa wazazi na wanafunzi wanaotegemea kujiunga na vyuo vikuu kwa mwaka husika juu ya programu zinazotolewa na vyuo hivyo pamoja na kutoa ushauri ni programu gani mwanafunzi asome kwa kuangalia ufaulu wake.

JWTZ Wapo Tayari Kukabiliana Na Ugaidi Afrika


Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema lipo tayari kukabiliana na ugaidi nchini na kwingineko barani Afrika. 

Kwa wiki mbili mfululizo, askari wa JWTZ waliungana na majeshi ya nchi nyingine nane kufanya mafunzo maalumu ya kukabiliana na ugaidi, biashara ya dawa za kulevya, usafirishaji wa binadamu na uharamia. 

Akitoa tathmini, Mkurugenzi wa Mazoezi hayo, Brigedia Jenerali Yohana Mabongo alisema yameenda vizuri na askari wamepata fursa ya kufahamiana na kubadilishana uzoefu. 

“Tupo vizuri. Tunaweza kukabiliana na uhalifu wa kimataifa, ndani na nje ya Tanzania,” alisema Brigedia Jenerali Mabongo. 

Alifafanua kuwa awali askari walikuwa wanafanya kazi kiutamaduni wakiwa na lengo la kulinda mipaka kwa kutumia silaha nzito, lakini kutokana na kubadilika kwa tishio la usalama, majeshi mengi duniani yameona kuna haja ya kuwa na mbinu mbadala. 

“Kupambana na gaidi au mtuhumiwa wa dawa za kulevya hakuhitaji kifaru au mzinga. Majanga yanayoletwa na mapigano au mashambulizi ya kushtukiza huacha athari nyingi kwa jamii ambazo hustahili msaada. 

"Tutayafanya hayo yote hapa nchini au popote Umoja wa Afrika (AU) utakapoona kuna haja ya kufanya hivyo,” alisema. 

Mafunzo hayo yanayoshirikisha raia kutoka AU, Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na Shirika la Msalaba Mwekundu yanafadhiliwa na Tanzania na Marekani. 

Jana, Balozi mdogo wa Marekani nchini, Virginia Blazer alitembelea Chuo cha Mafunzo ya Kuimarisha Amani Tanzania (TPC) Kunduchi na kupokea ripoti ya utekelezaji.

Uganda, Djibouti na Ethiopia ni miongoni mwa nchi zinazoshiriki mafunzo hayo. 

Kwa muda mrefu, Uganda inakabiliana na Joseph Kony anaeendesha mapigano ya kisasi kaskazini mwa taifa hilo na alipoulizwa juu ya mchango wa mafunzo hayo, Kiongozi wa askari wa Jeshi la Uganda (UPDF), Kanali Fred Twinamatsiko alisema jeshi hilo lipo tayari wakati wote, lakini kuna changamoto za kufanikisha suala hilo. 

“Utayari wa kisiasa ndiyo unaokosekana. Mara nyingi tumempiga Kony na kumuondoa alipokuwapo. Endapo wakubwa watakuwa tayari, UPDF inamuondoa muda wowote,” alisema.

Nyayo za Lowasa Zinaweza kutikisa Kikao cha CCM Dodoma

Image result for lowassa
Wakati CCM ikijiandaa kumkabidhi Rais John Magufuli uenyekiti, suala la masalia ya Edward Lowassa linaweza kuchukua nafasi kubwa katika vikao vitatu vya juu vinavyofanyika kwa mara ya kwanza tangu kumalizika Uchaguzi Mkuu mwaka jana. 

Ni dhahiri kuwa Mkutano Mkuu Maalumu ulio na ajenda moja tu ya kumchagua mwenyekiti mpya hautakuwa na nafasi ya kujadili ajenda nyingine, lakini Halmashauri Kuu iliyogawanyika baada ya Lowassa kuenguliwa kwenye mbio za urais, inaweza kuchukua muda kujadili CCM mpya baada ya waziri huyo mkuu wa zamani kujiondoa Julai 28 mwaka jana.

CCM itaanzia mikutano yake kwa kikao cha Kamati Kuu, ambayo hufanya maandalizi ya kikao cha Halmashauri Kuu kitakachofanyika Ijumaa na kumalizia na Mkutano Mkuu Jumamosi wiki hii.

Pia kutakuwa na kikao kingine cha Halmashauri Kuu kitakachofanyika Jumapili ambacho kwa sehemu kubwa kinatarajiwa kujadili taarifa za wasaliti zilizoandaliwa na kamati za siasa za mikoa na huenda kikatoa maamuzi mazito yanayobeba mustakbali wa kuijenga “CCM ya Magufuli”.

Lakini makada wengi waliohojiwa  kuhusu suala la masalia ya Lowassa kuibuka kwenye vikao hivyo, walipinga wakisema waliomuunga mkono mwanasiasa huyo maarufu, walifanya hivyo wakati akiwa CCM na kwa kuwa hawakumfuata hawatarajii suala hilo kuibuka tena.

“Makundi ndani ya CCM yalikwisha baada ya Magufuli kupitishwa kukabidhiwa kijiti,” alisema mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Geita na mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Msukuma alipoulizwa kuhusu suala la Lowassa kuibuka kwenye vikao hivyo vya juu.

Msukuma, ambaye alifanya mbwembwe za kuhama kambi ya Bernard Membe kwa kutua na helikopta kwenye mkutano wa Lowassa mjini Arusha, alisema wakati CCM ikisaka mgombea wake wa urais, kulikuwa na makundi zaidi ya 40.

“Wakati ule kila mgombea alikuwa na kundi. Ila kwa sasa sidhani kama hali hiyo bado ipo maana baada ya mgombea kupatikana kila mmoja alimuunga mkono,” alisema Msukuma.

Kauli kama hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida ambaye alisema kila mwenyekiti huja na timu yake, hivyo kama kutakuwa na mageuzi, si kitu kinachohitaji mjadala. 

“(Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin) Mkapa alipomuachia uenyekiti (Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya) Kikwete alikuja na timu yake mpya. Kama utakumbuka katibu mkuu wake alikuwa Yusuf Makamba,” alisema Madabida ambaye naye alikuwa miongoni mwa wenyeviti waliomuunga mkono Lowassa.

“Nina matarajio na rais. Naamini atakifanya chama kuwa imara zaidi na kuleta mageuzi ya kisiasa na kiuchumi. Mabadiliko ni kawaida na wenyeviti wapya huja na kamati kuu na sekretarieti mpya.”

Hata hivyo, kuanzia Januari mwaka huu kamati za siasa za mikoa zimekuwa zikikutana kujadili watu wanaoitwa ni wasaliti na kupeleka mapendekezo ya hatua dhidi yao kwenye vikao vya juu.

Rais Magufuli, ambaye hajawahi kushika uongozi wa chama, anaaminika kuwa ataifanya CCM kuwa na sura, mwelekeo na ushawishi mpya, hali itakayochangia kukata mizizi iliyojengwa na wanasiasa mashuhuri.

Kutokana na hali ilivyokuwa wakati Lowassa akiondoka CCM na mtikisiko aliouacha, chama hicho hakitaweza kujipapatua bila kumtaja Lowassa na mtandao wake wakati kikijadili jinsi ya kusonga mbele.

Mbunge huyo wa zamani wa Monduli amekuwa akijadiliwa kwa ushabiki mkubwa ndani na nje ya vikao halali vya CCM tangu alipojitokeza kwa mara ya kwanza mwaka 1995 kuwania urais akiwa na umri wa miaka 42.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, mwanasiasa huyo aliwagawa makada wa CCM na alipohamia Chadema kuna kundi lilimfuata na jingine kubakia, huku baadhi ya wanachama kwenye kundi hilo wakituhumiwa kwa usaliti.

Baada ya kujiondoa CCM Julai 28, 2015 na kujiunga Chadema alikoteuliwa kuwa mgombea urais na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), mashambulizi mengi kutoka CCM yalielekezwa kwake.
 
Vikao vinavyosubiriwa kutia muhuri mapendekezo ya kamati za siasa za mikoa ndivyo vinavyofanyika wiki hii mjini Dodoma baada ya CCM kuitisha mkutano mkuu maalumu ili kukamilisha taratibu za kumkabidhi Rais Magufuli usukani wa chama hicho.

 Halmashauri Kuu ya JPM 
Halmashauri Kuu ya JPM inatarajiwa kutumbua watendaji wazembe, goigoi, wasiokwenda na kasi yake, wabadhirifu wa fedha za chama na wengine ambao uwapo wao ni mzigo kwa CCM.

Hivyo, Halmashauri Kuu itasuka upya chama, pia kwa kujaza nafasi za watendaji waliojiuzulu kutokana na desturi ya chama hicho.

Kwa kawaida, CCM inapopata mwenyekiti mpya, sekretarieti yote hujiuzulu ili kumpa nafasi kiongozi huyo kupanga safu yake, alisema msemaji wa chama hicho, Christopher Ole Sendeka juzi alipoongea na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Sekretarieti inaongozwa na katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ambaye anaaminika kuwa alifanya kazi kubwa ya kukirudishia chama hicho nguvu wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu uliopita ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Wengine ni Vuai Ali Vuai (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar), Rajab Luhavi (Naibu Katibu Mkuu Bara), Mohamed Seif Khatib (Katibu wa Oganaizesheni) na Nape Nnauye (Katibu wa Itikadi na Uenezi).

Wengine ni Dk Asha-Rose Migiro (Katibu wa Idara ya Mambo ya Nje), na Zakia Meghji (Katibu wa Uchumi na Fedha).

Halmashauri Kuu ya JPM inatarajiwa pia kujadili hali ya hewa ya kisiasa ndani ya chama, kupanga mikakati ya kuimarisha uchumi na kutekeleza mapendekezo ya kuwafukuza wasaliti, ambao wanatuhumiwa kuwa waliendelea kumuunga mkono Lowassa wakati wa kampeni na kusababisha chama kupoteza baadhi ya majimbo.

 Oktoba 30, 2015 baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi wa urais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva iliandaliwa hafla fupi makao makuu ya CCM Lumumba, ambako Dk Magufuli alimwambia mwenyekiti wake akisema: “Umezungukwa na wanafiki na watu ambao ulidhani watakusaidia kwenye chama, lakini wamekuangusha”  

Miongoni mwa watu ambao hata wakati wa kampeni alikuwa anawashutumu ni waliowahi kushika nyadhifa za juu serikalini, lakini wakahamia upinzani na kuibeza Serikali.

 Dk Magufuli anaonekana alikuwa anawalenga Lowassa na mwenzake Frederick Sumaye ambao waliunda safu kabambe ndani ya Chadema kuisakama CCM.

Orodha ya watakaotumbuliwa na NEC ya JPM ni ndefu. Baadhi yao ni makada waliojitokeza hadharani kupinga utaratibu uliotumiwa na wazee kukata jina la Lowassa kugombea urais. 

Hata baada ya CCM kumteua Dk Magufuli kuwa mgombea urais, bado wapo waliompinga wakidai hana mizizi katika chama.

Wengine wanaoweza kutumbuliwa ni walioanzisha wimbo wa “Tuna imani na Lowassa” ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wakionyesha utiifu wao kwa Lowassa badala ya Mwenyekiti Kikwete aliyeongoza kikao cha Kamati Kuu kilichotoa majina matano ya waliopitishwa kugombea urais bila ya jina la Lowassa kuwamo.

Wengine wanaoweza kutupiwa virago ni makada waliosusa kumpigia debe Dk Magufuli pamoja na waliodaiwa kukitelekeza chama.

Habari nyingine zinasema waliopendekezwa kufukuzwa na vikao vya wilayani ni wanaodaiwa kubadilika usiku na kusaidia Ukawa, wakiwamo wenyeviti wa mikoa na makatibu.

Pia, wamo baadhi ya wabunge na wafanyabiashara waliokuwa wanawabeba mamia kwa makumi ya wanachama kwenda nyumbani kwa Lowassa mjini Dodoma kuonyesha kumuunga mkono
Older Posts
© Copyright UHURU WA MAWAZO | Designed By Code Nirvana
Back To Top